Na Esther Macha ,Rungwe
MKUU wa Mkoa wa Mbeya ,Albert Chalamila ametoa wiki moja kwa uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe kukamilisha upanuzi wa chumba cha kuhifadhia maiti pamoja na
jengo la kufulia nguo katika kituo cha afya Ikuti ambacho ujenzi wake umeonekana kusuasua licha ya serikali kutoa fedha .
Mkuu Huyo wa Mkoa alisema hayo Jana wakati wa ziara yake ya kukagua kituo hicho cha afya kilichopo wilayani humo.
Aidha Chalamila alimwagiza Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Loema Peter kufuatilia kwa makini kama kweli mafundi ujenzi wanaojenga majengo hayo kama wamelipwa fedha zao .
"Kumekuwa na tatizo la ukorofi .kwa mafundi wakuu kutowalipa fedha mafundi wadogo Mkurugenzi angalia hili"alisema Mkuu wa Mkoa.
Alisema mashine hizo zilizoletwa na serikali zimekaa nje kwa miezi.mitatu hili liwe la mwisho na halivumiliki.
Aidha Chalamila alisema kutokamilisha vituo vya afya ni uzembe mkubwa hasa ukizingatia fedha hizi zimetolewa na serikali kwa muda mrefu sana na kuwa viongozi wakiwa wakweli ujenzi ungekuwa umekamilika.
"Leo nimekuja kutoa onyo la kwanza lakini kwakuwa mnaendelea na kazi siwezi kusema chochote ila siku ya ijumaa endapo nitakuja majengo yakiwa hajakamilika nitachukua hatua kubwa mh Rais magufuli ametoa fedha hizi kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya lakini kwa kitendo hiki cha kusuasua kinatia uchungu sana "alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Mkuu wa wilaya ya Rungwe ,Julius Chalya alisema kilichopo kwa ujenzi wa vituo vyote hivyo ni uzembe na usimamizi mbovu pamoja na usikivu wa kutozingatia maelekezo wa ujenzi wa vituo vya afya.
Alisema Mkurugenzi ndio alitakiwa kusimamia ujenzi huo lakin cha ajabu mafundi walifanya Nazi kiholela na mpaka diwani nae kutafuta mafundi wake.
Akitoa ufafanuzi wa ujenzi huo,Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo ,Loema Peter alisema kwamba sababu ya kuchelewa kuanza ujenzi huo ni kutokana na fedha za ujenzi wa hospitali ni mapato ya ndani na kuwa taratibu zinachukua muda mrefu.
Aidha Mkurugenzi huyo alisema kuwa huo si muda wa kulaumiana halmashauri imeleta.mil50,ili kuendeleza ujenzi huo na kama tukiendelea kukwaluzana nani kafanya nini hatuwezi kufika popote.
Naye Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe ,Ezekiel Mwakota alisema Mkurugenzi wa halmashauri asijitete kabisa maagizo yanayotolewa na serikali yawe yanafanyiwa kazi yasisubiri uongozi wa juu unapokuja ndo wanaanza kufanya.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa