Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. AmosMakalla amewapongeza wananchi wa Kata ya Madibira wilani Mbarali kwa kazi kubwawalioifanya ya kuweza kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa 3, Ofisi ya Walimu1, bweni na vyoo katika shule ya Sekondari ya Madibira.
Mkuu wa Mkoa ameyasema hayowakati wa ukaguzi wa ujenzi wa madarasa Wilaya ya Mbarali ili kuhakikisha vyumbavya madarasa vinakamilika na wananafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na Kidatocha kwanza wanaripoti shuleni kwa ajili ya kuendelea na masomo.
Mhe.Makalla amesema kwamba Wilayaya Mbarali ndio ilikuwa na Idadi kubwa ya wananfunzi ambao wanafunzi 4200walishindwa kujiunga na Elimu ya Sekondarii kutokana na uhaba wa madarasa naujenzi wa vyumba vya madarasa 39 ukikamilika wanafunzi wote wataripoti shule.
Akisoma Taarifa ya Ujenzi Mkuu waShule ya Sekondari ya Madibira Mwl. John Gwimile amesema kuwa ujenzi wabweni yawanafunzi unatarajiwa kukamilika tarehe mwezi Februari 15 na kwa sasa wanafunziwa Kidato cha sita wanatumia vyumba vya madarasa kama mabweni.
“Yatakapo kamilika mabweni hayawanafunzi wa Kidato cha Sita watahamia na kuacha wazi madarasa wanayotumia kamamabweni kwa ajili ya wananfunzi wa Kidato cha kwanza. Shule itakuwa imepunguzauhaba wa madarasa kwa ajili ya wanafunzi walioshindwa kujiunga.” Mwl Gwimile
Mwl Gwimile amesema kuwa bwenihilo linagharimu shilingi milioni 75 ambapo michango ya wananchi ni shilingimilioni 17 na fedha nyingine ni kutoka Serikalini Mbweni hilo litakuwa na uwezowa kuhudumia wanafunzi 96,
DiwaniKata ya Madibila Mh.Erick Ngeliama alimshukuru Mh Mkuu wa Mkoa na uongozi waWilaya kwa kuja kutembeleaKata ya Madibila, na kusisitiza kuwa Maendeleohayana Mtu furani, itikadi,rangi, dini wala chama kwani tutakuwa tunakoseatukifuata utaratibu huo, nijambo la faraja kuona watoto wote wanakwenda shulebila kuangalia anaesimamiamaendeleo ni nani, cha msingi ni kuweke siasapembeni na kufanya kazi.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa