Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila amewataka Watendaji wa halmashauri kutafakari kwa usahihi mipango na njia za kukabiliana na tatizo la kushuka kwa mapatio katika maeneo yao.
Akiongea leo baada ya kukabidhiwa Ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Chalamila amesema kuwa ni lazima halmashauri zifikirie njia sahihi za kuongweza mapato ya ndani.
Chalamila amesema kuwa moja ya mikakakti yake ni kuona namna halmashashauri hasa ya Jiji inakuwa na mipango ya kuinua ukusanyaji wa mapato ya ndani.
Aidha, amesema mikakati mengine ni kuona namna ya kudhibiti ajali za barabarani kwa kuwashirikisha Wadau ili kupunguza ajali zinazotokea mara kwa mara.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Amos Makalla alianza kwa kumponge Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa uteuzi aliopata na kumweleza kuwa Mbeya ni Mkoa mkubwa wenye fursa nyingi za Kiuchumi.
Mhe. Makalla akasema kuwa kuna migogoro sita ya ardhi ambayoa ameiacha na inahitaji utekelezaji wa haraka ikiwa ni maagizo ya Makamu wa Rais na migogoro hiyo inajumuisha Upanuzi wa Hifadhi Mbarali, Hifadhi ya Kitulo,Viwanja vya CCM, mgogoro wa Ilolo, upanuzi wa barabara ya Kikusya-Matema na Mgogoro wa ardhi Itezi,Ilemi na Mwakibete
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa