Na Godfrey Kahango
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila amesema viongozi waliopewa dhamana kuisimamia Serikali wakiacha ubabaishaji na kuendekeza rushwa na ufisadi, dhamira ya Rais John Magufuli kuwa Paris huduma nzuri wananchi itafanikiwa.
Mhe Chalamila ametoa kauli hiyo leo Jumatano Juni 12, 2019 baada ya kukagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Mbeya inayojengwa eneo la Inyala huku akiridhishwa na kazi ya Ujenzi huo uliogharimu sh. 1.5 bilioni.
“Magufuli ana dhamira nzuri na kubwa kwa Watanzania. Lakini niseme sisi viongozi aliotuamini tukiwa ‘wasabi’ katika kutekeleza maazimio yake hatutamuwakilisha vizuri”.
“Lakini tukiacha ‘usanii’ na kuweka kando ufisadi na rushwa tutamwakilisha vyema katika kuwahudumia wananchi wetu ,” Amesema Mhe Chalamila
Amebainisha Ujenzi wa hospitali tatu za Halmashauri ya Mbarali, Busokelo na Mbeya pamoja na Vituo vya Afya 14 utagharimuzaidi ya sh. bilioni 11.2, kubainisha kuwa unaendana na a hizo la Serikali kutaka hospitali zote ziwe zimekamilika kabla ya Juni 30, 2019
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Steven Katembo amesema kiasi hi hicho cha fedha kimetumika kujenga majengo saba ya hospitali hiyo lakini sh milioni 60 zilitolewa na halmashauri yake zitajenga majengo mengine mawili ambayo ni nyumba za watumishi.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika amesema kukamilika na kuanza kutumika kwa hospitali hiyo kutakuwa msaada kwa zaidi ya wananchi wa maeneo hayo na maeneo ya Jirani.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa