Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila ametoa zawadi ya bati bando 250 sawa na bati 3000 aina ya Simba yenye thamani ya shilingi milioni 74 kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Mbeya.
Mhe Chalamila ametoa mabati hayo leo kwa wakurugenzi wa Halmashauri hizo na kusema kuwa watoto waliofaulu wapo 34,403 na waliopata nafasi wapo 28,148 tu sawa na asilimia 81.82%. Wanafunzi ambao tunadaiwa pahali pao pa kusomea wapo 6225 Kwa mkoa mzima sawa na madarasa 143.
Amesema kuwa ameona ni vema kuchangia mabati hayo kutoka Alafu aluminum ili yaweze kuezeke madarasa ambayo wazazi wa kipato cha chini na wenye uwezo wamechangia hadi kufikia hatua ya hii.
Mhe Chalamila amesema mabati hayo yametumia kiasi cha milioni 74.6 Kwa faida ya watoto wetu. Nawaomba sana sana tuendelee kuhamasishaa maendeleo na kukataa mgawanyiko usio na tija Kwa taifa.
Chalamila amesema kuwa Mh Rais John Magufuli ameanzisha mwendo wa elimu bila malipo kwa shule za sekondari na msingi kama ilivyokuwa. Ni wajibu wetu kuunga mkono juhudi hizo kwa vitendo.
Amesema kuwa Usajili mkubwa wa wanafunzi umetokana na Kauli mbiu ya Mh Rais ya Elimu bure. Kila mwezi zaidi ya 23bilioni zinaletwa mashuleni.
Chalamila amewataka watu wote wenye mapenzi mema na mkoa wetu na TANZANIA kujitokeza kuchangia maendeleo kwa maslahi ya Taifa. Ukiwa na uwezo kajenge darasa,vyoo, madawati, meza za walimu, cement, mchanga, nk peleka kwenye shule yoyote unapoona panafaa.
Amesema kuwa katika kufanya hivyo wakuu wetu wa shule, waratibu na Maafisa elimu wanajua taratibu na kanuni za uchangiaji. Usisite kuwauliza Njia bora ya kufikisha mchango wako.
Elimu bora Kwa watoto wetu inawezekana. Watoto wa masikini kupata elimu ya sekondari inawezekana.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa