Naibu Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson amekabidhi mradi wa jengo
la upasuaji katika kituo cha Afya Ruanda lililokarabatiwa
na Taasisi ya Tulia Trust kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Amos Makalla
lililogharimu Sh. milioni 40.
Dkt Tulia amekabidhi jengo hilo katika ziara yake mkoani hapa
sambasamba na kukagua ukarabati wa mradi huo na kuzungumza na
wananchi na wagonjwa waliofika kupata matibabu katika kituo hicho.
Amesema katika kuunga mkono jitihada za Serikali taasisi yake
imelenga kuboresha huduma muhimu hususan afya, hususan huduma ya
wakinamama wajawazito na watoto katika vituo vya afya na zahanati.
"Mkuu wa Mkoa nakupongeza kwa jitihada zako mpaka kufikia hatua za
mwisho za kusimamia mradi huu sasa ninaomba changamoto za mahitaji
madogo yaliyopo yafanyiwe kazi ili huduma za upasuaji zianze
kutolewa"amesema.
Mkuu wa Mkoa Amos Makalla, alisema kuwafuatia Serikali imetoa Sh 700
milioni kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya kisasa katia kituo cha afya
Ruanda pamoja na vifaa tiba.
"Naibu Spika ukarabati wa chumba cha upasuaji imekuwa chachu kwa
serikali na sasa imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya kisasa
katika kituo hiki kwa kweli unatupa moyo sana kama viongozi wa
Mkoa"amesema.
Aidha ameagiza halmashauri ya jiji kupitia mapato yake ya ndani kutoa
fedha kwa ajili ya kumalizia baadhi ya mahitaji katika chumba cha
upasuaji ili kianze kutoa huduma kwa wananchi.
"Natoa wiki mbili ukarabati huu uwe umekamilika na huduma zianze
kutolewa mapema iwezekanavyo"amesema.
Mganga mfawidhi katika kituo hicho, Elioth Sanga alisema wametenga
Sh 55 milioni kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya upasuaji.
Kwa upande wa Mdau wa Mendeleo Mkoani hapa, Ndele Mwaselela alisema
anaumba mkono jitihada za serikali katika kuhakikisha wanaboresha afya
za msingi kwa kuchangia miradi ya maendeleo hususan elimu na afya.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa