Wananchi Mkoani Mbeya wamesema kitendo cha Serikali kununua Mpunga kwa bei ya juu kuliko wanunuzi wa kawaida kimeleta chachu na ari ya kuendeleza kilimo kwa kuwa mbali na manufaa ya kipato kuwa kikubwa lakini pia imeongeza ajira kwa Vijana na wanawake.
Wakiwa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera aliyefika kwaajiri ya Uzinduzi wa kituo cha kuuzia Mpunga cha Uturo wananchi wameweka wazi juu ya ubora wa bei za Serikali ambapo gunia la kilogram g100 wanauza kwa shilingi 110,000/= sawa na shilingi 1,100/= kwa kilogramu 1 tofauti na wanunuzi wengine wanaonunua kwa elfu 80 kwa gunia la kilgramu 100 sawa na shilingi 800 kwa kilogram 1.
Akizindua kituo hicho cha Utulo kilichoko Wilaya ya Mbarali kwa niaba ya vituo vingine vya mkoa wa Mbeya, RC Homera amesema bilioni 37 zilizotengwa na Serikali zitakazonunua tani elfu 31 za Mpunga watahakikisha zinafanya kazi iliyokusudiwa ya kumkwamua Mkulima na Mazao yake.
Vituo vingine vitakavyonunua Mpunga kwa Mkoa wa Mbeya mbali na Utulo ni Madibila, Makwale (KYELA) na vituo viwili vitakavyofunguliwa hivi karibuni ni Kapunga na Ubaruku vyote vipo Wilaya ya Mbarali.
Kwa Upande wake Kaimu Meneja wa Wakala wa hifadhi ya Chakula Taifa NFRA kanda ya Songwe CPA Eva Michael ameahidi kuendeleza ushirikiano na Wakulima wote wa Mkoa wa Mbeya kadharika Kanda nzima ya Songwe.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa