Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama imefanya ziara katika Gereza la Kilimo la Songwe kwa lengo la kukagua shughuli zinazotekelezwa na Gereza hilo na kuongea na wafungwa.
Akisoma taarifa kwa Kamamti ya Bunge Mkuu wa Gereza la Songwe ACP Lyzeck Mfaume Mwaseba amesema kuwa Gereza la Songwe ni la kilimo ambapo kwa mwaka 2016/2017 wana matarajio ya kulima ekari 300 Mahindi, 40 za Alizeti, 10 mboga mboga na matunda na ekari 50 kwa ajili ya kilimo cha Umwagiliaji.
Hata hivyo Bw. Mwaseba amesema kuwa bado kuna changamoto ya uhaba wa vitendea kazi kama matrekta kwa ajili ya kilimo na magari ya kuwasafirishia wafungwa hivyo kupelekea gereza kutofikia malengo yake ya kilimo kama lilivyotarajia kutokana na uchakavu wa vifaa vilivyopo.
Aidha,Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amesema kuwa Jeshi la Magereza Mkoa linatakiwa kujipanga kwa kuomba mikopo ya vitendea kazi kwenye taasisi za Serikali ili waweze kutimiza malengo yao.
Naye, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Kanali Mstaafu Masoud Ally amewataka viongozi wa Magereza kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kutokatishwa tamaa na changamoto ndogo ndogo zinazojitokeza.
Wakati huo huo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ilipata nafasi ya kutembelea na kukagua mipaka ya Tanzania na Malawi wilaya ya Kyela
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa