Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila aamuru kuwekwa ndani masaa 24 Diwani wa Kata ya Isanga Amon Mwalwiba (CHADEMA) na Mtendaji wa Kata Ndg Robin Nzowa kwa tuhuma za ubadhilifu wa fedha zilitolewa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa ajili ya Ujenzi wa vyoo shule ya Msingi Ilolo.
Mhe Chalamila ameagiza hayo leo kwenye mkutano wa hadhara Kata ya Isanga baada ya wananchi wa kata hiyo kulalamikia matumizi mabaya ya fedha hizo kupelekea mradi wa ujenzi wa vyoo vya shule ya Ilolo kutokamilika mpaka sasa.
“Hoja walizozitoa wananchi ni za msingi, OCD kamata Diwani na Mtendaji ili wakatoe maelezo ya matumizi ya fedha hizo na naunda tume ya wataalamu ambao kesho watakuja kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha na jengo” amesema Chalamila
Mhe Chalamila amesema kuwa pamoja na kuwaweka ndani ikidhibitika kama kweli wamrtumia fedha hizi kinyume na taratibu hatua kali za kisheria zitachukuliwa juu yao.
Ofisa Elimu Kata ya Isanga Israel Obed amesema halmashauri ilitoa sh, 2.5m kwa ajili ya ujenzi wa vyoo shule ya msingio Ilolo baada ya vyoo vya awali kuharibika na hakuna mjumbe kutoka baraza la kata aliyeshirikishwa katika matumizi ya fedha hizo.
Obed amesema katika kuhoji matumizi ya fedha hizo Mtendaji wa kata alikiri kutumia shilingi 460,000 kwa matumizi yake binasfi na kuomba muda wa wiki mbili kutafuta na kuzirudisha na fedha kiasi cha sh. 1.4m hazikutolewa majibu ya matumizi yake na diwani.
Akijibu tuhuma hizo Mtendaji wa Kata Nzowa aliahidi kuzirudisha fedha hizo kwenye akaunti ya kata.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Ilolo Bibi Shukuru Mbogela amesema hakuhusishwa katika ujenzi wa vyoo katika shule yake lakini alipokea malalamiko ya mafundi kutokulipwa fedha za ujenzi na baadhi ya vifaa vya ujenzi.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa