Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amewaagiza Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Mbeya kufanya uchunguzi wa ubadhirifu wa Sh800 milioni za chama cha akiba na mikopo cha walimu mkoani Mbeya.
Mhe Chalamila ameyasema hayo leo Jumamosi Desemba 4, 2020 kwenye mkutano wa 18 wa kupokea taarifa ya bodi ya SACCOS hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Kiwira.
Chalamila alitoa agizo hilo baada ya walimu zaidi ya 300 kumweleza kilio chao cha muda mrefu kwamba fedha hizo zimetafunwa na viongozi waliomaliza muda wao.
Mwalimu, Daniel Mwambapa alimuomba Chalamila kuwachukulia hatua viongozi hao na kwamba wamepeleka taarifa Takukuru zaidi ya mara tatu na hakuna matumaini.
"Mkuu wa Mkoa tumepeleka malalamiko Takukuru hakuna majibu tunayopata tunaomba ingilia kati kwani tunashangazwa tunakatwa makato benki wakati hatuna mikopo,” amesema.
Kufuatia Kauli hiyo Chalamila amesema huenda Takukuru walihusika akihoji sababu za tukio hilo kutoshughulikiwa na kutaka majibu hayo Desemba 7, 2020.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa