Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Albert Chalamila amewaagiza askari wote watakaokuwa wanaendesha zoezi la kuwakamata watu wanaoingia nchini kwa njia za panya mpaka wa kasumulu kutembea na panga na shoka kwa ajili ya kupasua mitumbwi inayotumiwa na wahamiaji hao.
Akiongea na wananchi na Viongozi wa Serikali Wilaya ya Kyela katika mpaka wa Tanzania na Malawi eneo la Kasumulu Mhe Chalamila amesema mpaka huo una vivuko visivyo rasmi zaidi ya 30 ambavyo wananchi wanavitumia kuvuka ili kukwepa kuwekwa karantini.
”Hivi vivuko visivyo rasmi ndivyo vinatajwa kutumiwa kuvuka kwa kificho hususani katika kipindi hiki ambacho sisi Serikali ya Mkoa wa Mbeya tunasimamia watu wote wanaoingia nchini kutoka nchi jirani kuwekwa karantini kwa siku 14 ikiwa ni sehemu ya kukinga kusambaa kwa maambukizi ya ugonjwa wa COVID 19”.Amesema Chalamila
Awali kwa Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya Mama Claudia Kitta amesema kuwa baada ya msimamo wa Serikali wa kuwaweka karantini, baadhi wakazi katika maeneo jirani na Mto Songwe unaotenganisha nchi ya Tanzania na Malawi wanatumia mitumbwi kuwavusha wageni kutoka nje ya nchi kupitia vivuko visivyo rasmi hatua ambayo inaleta ugumu wa usimamizi wa kubaini wageni.
Mama Kitta alisema kuwa tayari wapo watu waliokamatwa wakivushwa mpaka kwa kutumia mitumbwi ambapo wanaendelea kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa wanachukuliwa kama wahamiaji haramu.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa