Na Esther Macha ,Rungwe
UJENZI wa majengo saba ya kituo cha afya cha Masukulu kilichopo wilayani Rungwe umeingia dosari baada ya kubainika majengo hayo kujengwa chini ya kiwango .
Lakini pia Vifaa vilivyonunuliwa vilikuwa tofauti na vilivyoidhinishwa kwa ujenzi wwa majengo ya serikali.
Akizungumza Jana Mara baada ya kutembelea ujenzi wa majengo saba ,Mkuu wa Mkoa wa mbeya Albert Chalamila alisema katika ujenzi huo wa majengo hayo kuna wizi mkubwa umefanyika .
Chalamila alisema kituo hicho cha afya cha masukulu ni mfano mchache wa vituo vya afya ambacho kimefanywa kuwa shamba la bibi.
"Nilitaka kufanya maamuzi hapa lakini mpaka nikasome taarifa ya Takukuru niliyoletewa nitarudi tena hapa kwenye kituo hiki baada ya siku nne na kwa hali hii lazima tuwawajibishe haiwezekani kabisa Mhandisi halmashauri hajitambui na hata msimamizi wa mradi huu hajitambui"alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Kwa upande wake Katibu tawala wilaya ya Rungwe ,Mnkondo Bendera alisema kwamba kilichofanywa na wasimamizi wa ujenzi wa kituo hicho hakuna sababu ya kudanganyana kikubwa wakubali kuwa wamekosa katika mradi huo kwani kuna wizi wa wazi kabisa hapa Mkurugenzi hukwepi.
Naye Diwani wa kata ya Masukulu ,Weston Mwansasu alisema kilichofanywa kuchelewa kwa mradi huo ni mkurugenzi wa halmashauri kutowajibika katika nafasi yake kwani fedha za ujenzi huo wa majengo toka zimekuja zina miezi mitatu lakini hakuna kazi iliyofanyika mpaka pale taarifa ya ujio wa Mkuu wa mkoa ilipokuja ndio ujenzi ujenzi ulipoanza.
"Hali ya ujenzi ndio kama unavyoona upo chini ya kiwango kabisa hapa kulikuwa na wizi wa wazi kabisa katika.manunuzi na ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri"alisema diwani huyo.
Aidha Mwansansu alisema alipotaka kuhoji kama diwani aliambiwa kuwa ni maagizo kutoka ofisi ya Mkurugenzi kwani magari yaliyokuwa yanabeba mchanga baada ya kushusha wanaambiwa kuwa ni tripu tatu wakati ni moja tu ni wizi wa wazi kabisa.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe, Loema Peter alisema walipokea mil .500,kutoka serikali kuu kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha Masukulu pamoja na Ikuti mil.500 .
Mwisho.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa