Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Juma Zuberi Homera leo Mei 12 amefika Wilayani Kyela Mkoani Mbeya ambako kwa niaba ya Serikali ameweza kukabidhi misaada mbalimbali kwa wahanga waliokumbwa na mafuriko Wilayani Kyela.
Akizungumza na wananchi waliokumbwa na mafuriko hayo Homera amesema Serikali imetoa msaada wa Chakula na vifaa vya malazi kwa wananchi walio athirika na mafuriko Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya, baada ya kukumbwa na mafuriko kwenye kata za Mwaya, Ndandalo, Katumba songwe na kusababisha vifo vya watu watatu.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Michael Mumanga ambaye ni Mkurugenzi idara ya menejiment ya maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, amesema wamefikia hatua hiyo baada ya kupata maombi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya. Mumanga amesema misaada hiyo imetolewa na wadau mbalimbali wakiwemo msalaba mwekundu.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera amesema ili kudhibiti mafariko hayo Serikali ya Tanzania na Serikali ya Malawi wanatarajia kujenga bwawa la mto Songwe ambalo litasaidia kupunguza mafuriko
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa