Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Juma Zuberi Homera leo 13/06/2022 amekabidhi pikipiki 7 kwa warajisi wasaidizi wa vyama vya ushirika wa halmashauri zote saba za mkoa wa Mbeya. Tukio hilo limefanyika Jijini Mbeya ambazo zimetolewa na Tume ya Maendeleo ya Ushirika.
Akizungumza baada ya Kukabidhi pikipiki hizo Homera amesema lengo la kutolewa pikipiki hizo ni kurahisisha shughuli za ushirika katika maeneo husika na kuongeza ufanisi wa kazi kwa warajisi wasaidizi katika halmashauri zao.
“Dhamira kuu ya serikali ni kukuza ushirika katika Mkoa Wetu wa Mbeya, niwathibitishie tu kwamba tutaendelea kuinua ushirika na tutaendelea kutumia ushirika katika kuuza mazao yetu” Homera alisema.
Amewataka warajisi wasaidizi kutoka katika halmashauri 7 zilizopo Mkoa wa Mbeya kuzitunza pikipiki hizo na kuzitumia vizuri kwa shughuli za Serikali ili kuweza kuwasaidia katika utendaji wao wa kazi.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa