Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera amekutana na ujumbe wa Chama cha Madaktari Bingwa wa upasuaji Tanzania (TSA) ukiongozwa na Rais wa chama hicho Dkt. Larry O. Akoko na Mganga mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dkt. Salum Manyata pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji walipofika ofisini kwake leo jijini Mbeya.
Akizungumza na ugeni huo Homera amewashukuru wataalamu hao kwa kuja kutoa huduma za matibabu ya kibingwa katika kambi ya upasuaji inayofanyika katika hospitali ya Rufaa ya kanda Mbeya na kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi kwani gharama za matibabu hayo ni nafuu kulinganisha na kuzifwata huduma hizo jijini Dar es Salaam.
Homera ameahidi ofisi yake kutoa ushirikiano kwa chama hicho cha Madaktari bingwa wa upasuaji wakati wote wa utoaji wa matibabu kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya na Mikoa jirani kuweza kujitokeza kwa wingi ili kupata huduma hiyo.
Mkutano Mkuu wa 27 wa Chama cha Madaktari Bingwa wa upasuaji unatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 16 hadi 18 Juni mwaka huu jijini Mbeya.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa