Kamati ya Usalama ya Mkoa na Wilaya Mbeya imepiga marufuku bajaji zote kutoa huduma nje ya eneo waliloruhusiwa kwa mujibu wa leseni zao za Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Ardhi (LARTA)
Hayo yamesemwa na Comredi Juma Homera Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya Mkoa leo Mei 27, alipokuwa akisoma maazimio ya kamati kwa wadau wa usafirishaji wakiwemo wamiliki wa daladala, Pilipili, malori na bajaji katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Homera amesema kuwa vyombo vya usafiri vinatakiwa kuzingatia sheria na kanuni zinazowaongoza pale wanapokuwa wanatoa huduma kwa wananchi
“Ukienda LATRA pale wameanishiwa maeneo ya kufanyia kazi zao na vituo maalumu. Kwa hiyo daladala na bajaji wafanye biashara kwa mujibu wa leseni zao zinavyowataka” Homera
Maazimio mengine ni pamoja na bajaji kutoingia stendi ya Kabwe na Mwanjelwa, madereva bajaji kutopakia abiria kwenye vituo vya daladala ,pamoja na kutozidisha abiria watatu (3) kwenye bajaji wasiozidi kuwataka madereva bajaji kufuata taratibu za LATRA
Ameendelea kusema kuwa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa na Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) kuhakikisha wanafanya marekebisho ya barabara za pembeni ili kuendelea kupunguza msongamano barabara kuu
Aidha, Mhe Homera ameunda kamati ya kupitia na kusikiliza changamoto kutoka kwa wadau wa usafiri wa umma na wadau wa maendeleo Mbeya kuipa siku 10 kuanzia leo
Alhamisi Mei 27, 2021 kukamilisha kazi hiyo.
Homera amesema kuwa suala la migomo lina athari kubwa kwa jamii ikiwemo wanafunzi wa kike kukosa usafiri wa kuwafikisha shuleni hivyo kuwa katika hatari kubwa ya kupata mimba.
Naye Naibu Spika na mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini,Dk Tulia Ackson amesema amesikitishwa na kitendo cha kuchafuliwa na watu wachache kuwa yeye anamiliki bajaji zaidi ya 300 jambo ambalo ni la uzushi.
DkTulia amesema kuwa yeye hamiliki bajaji bali amekuwa akitoa mikopo kwa vijana kupitia taasisi yake ya Tulia Trust na kwamba anashangazwa na uzushi huo.
Dereva wa lori la mizigo,Elius Amangwinde alimeishauri Serikali kudhibiti utitiri wa vituo vya ukaguzi ambavyo vimekuwa kikwazo kikubwa cha utendaji wa kazi zao.
"Sisi madereva tunahitaji ushirikiano na Serikali kitendo cha utitiri wa vituo vya ukaguzi ikiwa na askari wa usalama barabarani kushindwa kudhibiti bajaji,pikipiki kwenye katika eneo la mataa ni aibu kubwa kwa madereva wanaotoka nje ya nchi.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa