Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Juma Homera ameiagiza Halmashauri za Mkoa wa Mbeya kunyanyua kiwango cha ufaulu kwenye shule za msingi na sekondari mpaka kufikia angalau asilimia tisini kwa vile jambo hilo linawezekana.
Mheshimiwa Juma Homera ameyazungumza hayo leo hii kwenye kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mkapa ambapo amewaagiza kuinua kiwango hicho cha ufaulu na kufikia angalau asilimia tisini (90%) kutoka kile cha awali cha asilimia 78% kwa shule za sekondari na asilimia (89%) kwa shule za msingi.
Aidha katika kuhakikisha kiwango cha ufaulu kinaongezeaka na kufikia lengo la asilimia tisini Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera ameweka bayana baadhi ya mikakati Ikiwemo kuandaa makambi kwa kila shule kwa ajili ya wanafunzi kujisomea na kufanya majaribio wiki mbili au tatu kabla ya mitihani ya mwisho, wanafunzi kufanya mitihani ya majaribio mara tatu kwa mwaka ambapo Halmashauri inatakiwa kugharamia zoezi hilo.
Pamoja na hayo Mkuu huyo wa Mkoa amezitaka Halmashauri zote mkoani humo kuunda dawati la kushughulikia kero za walimu na kuwasaidia kupata stahiki zao kwa wakati kwani kufanya hivyo kutawapa hali ya kufanya kazi kwa weledi na hatimaye kufanikisha kuinua kiwango cha ufaulu cha sasa nakufikia lengo la asilimia tisini linalotazamiwa.
Kwa upande mwingine Mheshimiwa Homera amewaagiza waratibu elimu kata kutembelea na kukagua maendeleo ya elimu kwenye kata zao ili kubaini changamoto na uzembe unaopelekea kukwamisha kiwango cha ufaulu kuongezeka na watakaobainika kufanya vibaya wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Juma Zuberi Homera ambaye ana wiki ya pili sasa tangu alipoapishwa amendelea kuwasisitiza watumishi hasa wakuu wa Idara mbalimbali katika Halmashauri za mkoa wa Mbeya kuwa wabunifu kwa vile ubunifu unasaidia kutatua changamoto na kupiga hatua kwenye maendeleo.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa