Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Comrade Juma Homera amewaomba waandishi wa Habari kuutangaza Mradi wa Bustani ya Starehe ya Jiji la Mbeya ambayo imewekezwa na Mwekezaji Maarufu kama Babito.
RC Homera amefika kutembelea Kituo hicho cha Starehe na Burudani cha Jiji la Mbeya Al-maarufu (MBEYA CITY PARK) na kuipongeza timu ya jiji kwa kufanya Makubaliano na Mdau Babito kuitengeneza Bustani hiyo ambayo itakuwa sehemu ya Uchangiaji mkubwa wa pato la Taifa.
Aidha ametoa wito kwa wawekezaji kuendelea kuwekeza Jiji la Mbeya na Mkoa kwa Ujumla na amewahakikishia kuwa maeneo yapo ya kutosha.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya Dormohamed Issa amesema Jiji litaendelea kutengeneza Mazingira ya Kuvitia Wawekezaji wengine ili kuendelea kutengeneza Upekee wa Jiji hilo na kiendelea kujiongezea Kipato kupitia Miradi ya Ndani.
Kwa Upande wake Babito ambaye ndiye Mwekezaji wa Kituo hicho amesema ujenzi unaendelea Vizuri na Muda si mrefu utakamilika na Wananchi wa Jiji la Mbeya na Mkoa Mzima wataanza kukitumia kituo hicho ambacho Wananchi wengi wanangona ukamilishwaji huo kwa hamu kubwa.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa