Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Juma Zuberi Homera leo ametembelea eneo la Inyala ambapo amezindua barabara ya mchepuko ambayo imetengenezwa kwa nia ya kupunguza ajali katika eneo hilo ikiwa ni siku chache baada ya kupokea maagizo kutoka kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango.
Maagizo ya Makamu wa Rais aliyatoa kwa wakala wa barabarani Nchini TANROAD juu ya kukamilisha ujenzi wa barabara ya mchepuo yenye urefu wa kilomita mbili kwenye mteremko wa pipe line kijiji cha Shamwengo kata ya Inyala, yametekelezwa baada ya kukamilika ujenzi huo.
Homera amesema Barabara hiyo iliyojengwa kwa ajili ya kutenganisha magari makubwa na madogo kwenye eneo la mteremko mkali ili kuweza kupunguza kutokea kwa ajali za mara kwa mara ambapo amewataka askari wa usalama barabarani kuwachukulia hatua madereva wote watakao kiuka maelekezo yao na hata wale wanaoendesha magari ya Serikali.
Meneja wa wakala wa barabarani Nchini TANROAD Mkoa wa Mbeya Mhandisi Matali Masige amesema Ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe umekamilika ndani ya siku nne, wakati ujenzi wa vituo vya kukagulia magari vikiwa vimekamilika kwa asilimia zaidi ya 70.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi Benjamini Kuzaga akitangaza Oparasheni kali kwa madereva wakaidi ambao watakua wakikiuka sheria kuchukuliwa hatua kali.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa