Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Juma Zuberi Homera, leo Machi 25, 2022 amezindua chanjo ya Ugonjwa wa Polio katika kata ya Ghana Jijini Mbeya hiyo ikiwa ni mara baada ya ripoti kuwepo kwa mlipuko wa Ugonjwa wa kupooza (Polio) katika Nchi jirani ya Malawi.
Kufuatia mlipuko huo, Uongozi wa Mkoa wa Mbeya umeandaa zoezi la utoaji chanjo kwa watoto wadogo chini ya umri wa miaka 5 iliyoanza kutolewa Machi 24 na zoezi litaendelea hadi Machi 27.
Polio ni ugonjwa unao waathiri Watoto wadogo wenye umri wa chini ya miaka mitano unaoenea kwa virusi na kumsababishia mtu kuathirika katika mfumo wa mishipa na kusababisha mtu kupooza.
Dalili zake ni pamoja na homa, kichwa kuuma, uchovu, kutapika, maumivu ya shingo na miguu.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa