Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Comrade Juma Homera leo Septemba 18 2023 amekutana na Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na kufanya nao Mazungumzo yaliyolenga kutambua Mchango wao katika Sector ya Afya hasa Katika ambapo moja ya Vitu alivyosisitiza ni Uadilifu na Nidhamu katika Utendaji Kazi.
"Hospitali yenu inafanya kazi Nzuri, inatoa huduma Nzuri na Wafanyakazi wenu wanahudumia Vizuri"
Aidha amewataka Wafanyakazi wa Hospitali hiyo kutunza Vifaa vya Hospitali vinavyotolewa na Serikali na kuepuka Matumizi mabaya na Uharibifu wa Makusudi
Kisha RC Homera akazungumzia swala la Ukusanyaji wa Mapato ambapo ameuasa Uongozi Kusimamia zoezi hilo la Vizuri na kutoa Ushauri kwa Wahudumu kuepuka kutumia Simu hasa kuperuzi Mitandao ya Kijamii wakati wanahudimia Wagonjwa.
Katika swala la Uwekezaji RC Homera amewaeleza Wafanyakazi wa Hospitali hiyo kuwa Wajitahidi kuwekeza kila wapatapo nafasi ya kupata chochote Katika sehemu ya Mapato yao kama Mishahara na posho ili kuepuka Utegemezi katika siku zao za Usoni
Dkt: Godlove Mbwanji Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya akamshukuru RC Homera kwa kutenga Muda wake kuzungumza na Wafanyakazi na kukitaja Kitendo hicho kama kitendo cha Kiungwana ambacho Viongozi wengine hawafanyagi hivyo. Viongozi wengine hawafanyagi hivyo.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa