Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Juma Zuberi Homera amepiga marufuku watumishi wa Serikali wanaopatiwa uhamisho kutoripoti kwenye vituo vya kazi bila kulipwa stahiki zao na kuonya waajiri kuachana na tabia hizo mara moja.
Homera amesema leo Jumapili Mei Mosi 2022 katika maadhimisho ya siku kuu ya Wafanyakazi ambayo kimkoa yamefanyika katika viwanja vya kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya.
Amesema kuwa Serikali imekuwa ikibeba mzigo mkubwa wa malimbikizo ya watumishi zikiwepo likizo na nyingine nyingi ambazo zinatokana na waajiri kushindwa kuwalipa kwa wakati.
Watumishi wote ambao kuanzia leo Mei Mosi atakayepatiwa uhamisho kwanza aende benki kuangalia kama ameingiziwa fedha na kama hazijaingia asiripoti katika kituo cha kazi.
Homera pia ameagiza Wakuu wa Wilaya na waajiri wote mkoani Mbeya kuhakikisha wanafanya vikao vya mara kwa Mara na watumishi ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero sambamba na kuacha wafanyakazi kuanzisha vyama vyao pasipo kukiuka misingi ya Sheria.
Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Dk Angelina Lutambi amesema kuwa serikali inatambua changamoto za watumishi na kwamba inaendelea kushughulikia kwa kadri itakavyoweza.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa