Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amepanga kuanza ziara ya kusikiliza kero za wananchi kila Wilaya mwezi wa nne ili kujiridhisha na namna madawati ya kero yanayosimamiwa na Wakuu wa Wilaya yanavyofanya kazi ya kuwahudumua wananchi wa maeneo yao.
Akiongea wakati wa kusikiliza kero za wananchi Ukumbi wa Mkapa Mhe. Makalla amesema kuwa ni miaka 2 tangu ameteuliwa aliweka utaratibu wa kusikiliza kero mara 2 kwa na kwa upande wa Wakuu wa Wilaya mara 4 kwa mwezi.
“Mwezi wa nne nitazunguka katika Wilaya zote kwa lengo la kujiridhisha na utendaji kazi wa madawati haya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa wakati na kuwa karibu na Serikali yao” alisema
Mhe Makalla amesema kuwa Mkoa wa Mbeya umekuwa mfano wa kuigwa kwa utaratibu uliojiwekea wa kutaka kuona wananchi wanahudumiwa vizuri kwa kusikiliza kero za wananchi kila alhamisi ya mwanzo wa mwezi na mwisho wa mwezi na kila alhamisi ya mwezi katika madawati ya kero wilayani.
Mhe. Makalla amesema kuwa utaratibu huu utapima uwajibikaji wa Watendaji wa Serikali katika nafasi zao kwa kutokuweka wigo kwa wananchi kutowafikia kwa urahisi.
Amesema wananchi wanatakiwa kuridhika na huduma wanazopata kwa kupunguza urasimu katika maeneo tunayofanyia kazi ili kupunguza malalamiko ya wananchi kwa Serikali yao.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa