Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila ameiagiza halmashauri ya Jiji kutotoza ushuru wafanyabiashara wadogo wenye vitambulisho vya ujasiriamali walipanga bidhaa zao kwenye vizimba ndani ya Soko Kuu la Mwanjelwa.
Mhe. Chalamila ameyasema hayo leo alipokuwa Akiongea na wafanyabiasha na wamachinga wa maeneo ya soko kuu la mwanjelwa, Bustani ya Sido na Kabwe na kusema kuwa Mhe. Rais alishafuta kodi hizo.
“Wale wote wenye vitambulisho vya ujasiriamali na wamepanga bidhaa zao kwenye vizimba ndani ya soko kuu la Mwanjelwa wasidaiwe fedha na Mkurugenzi ya ushuru wa vizimba ambayo ni 15,000 kwa mwezi na 500 kwa siku kwa kuwa fedha hiyo imefutwa”. Mhe. Chalamila
Awali Mhe Chalamila alianza kwa kusikiliza maoni ya wafanyabiashara namna ya kuboresha soko na kuvutia wateja na msongamano wa watu. Wafanyabiashara hao waliondolewa kwanye vibanda vya nje ya soko hilo na kuingizwa ndani
Bibi Zainabu Majid mfanyabiashara mdogo ameuomba uongozi wa Jiji kutengeneza mazingira maarufu kwa kuweka mgawanyiko wa bidhaa ndani ya soko hilo kwa sababu soko hilo halina wateja wengi na kukosa biashara kabisa na kushindwa kulipa ushuru wa kizimba kwa mwezi.
“Kuna hali ngumu sana kwenye soko hili, naomba nishauri halmashauri ya Jiji kuweka mgawanyo wa bidhaa kama tunaweza kuweka soko la mazao au soko la mitumba au bidhaa za ndani kama wanvyofanya soko la Kariakoo”. Bibi Majid
Naye Mkureugenzi wa Halmashauri ya Jiji Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, SSP James Kasusura…. Alisema atatekeleza maagizo hayo na wafanyabiashara hao hawatalipishwa ushuru wowote kutoka halmashauri ya Jiji.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa