Kikosi Kazi cha Kitaifa cha kunusuru mto Ruaha kimeagiza wawekezaji wa mashamba ya mpunga Wilayani Mbarali kusafisha mifereji ya matoleo ya maji kwenda Mto Ruaha ili kuongeza kiwango cha maji yanayoelekea katika bwawa la Mtera na Kidatu.
Wakiongea kwa nyakati tofauti Wajumbe wa Kikosi Kazi hicho wa,elaumu Wawekezaji wa Mahamba ya Madibira, Mbarali Estate na Kabunga Farm kuacha kwa makusudi kusafisha Matoleo ya Maji ambayo imejaa magugu maji na Masangu na kuzuia maji kutiririka kuelekea Mto Mbarali na Ruaha.
Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Jeeremia Minja ambaye ni Mjumbe wa Kikosi Kazi hicho amesema kuwa uchafu wa mifereji ya matoleo unasababisha Maji kutofika katika mto Ruaha na kusababisha upungufu wa maji katika Bwawa la Mtera na Kidatu hivyo kusababisha Upungufu wa uzalishaji wa umemem Kitaifa.
Bw. Minja amesema kuwa ni muhimu kuwachukulia hatua Wawekezaji wa mashamba hayo kwa kuwapiga faini kwa mujibu kwa kuisababishia Serikali hasara kubwa ya kuendesha mitambo ya umeme laini pia kwa kuzingatia sheria za mazingira.
Wakati huo huo Kikosi Kzi hicho kimesikitishwa na Wawekezaji hao kutolinda matoleo ya Maji yaendayo Mto Mbarali , Ndembele inayopelekea Maji Mto Ruaha na kuruhusu wananchi kuchepusha maji kwenda katika mashamba hayo bila kibali cha matumizi ya maji hayo.
Hii imepelekea Maji kutorudi katika Mto Ruaha na kuruhusu wananchi wa Wilaya ya Mbarali kutumia maji bila vibali ambapo inapelekea upungufu wa maji katika Bwawa la Mtera ambalo linauhitaji wa maji kwa wingi.
Aidha, Wawekezaji hao pia wameonekana kutofanya ukaguzi wa mazingira kwa ajili ya Kilimo kutokana na sheria ya mazingira ambayo inawapa Wawekezaji au watumiaji maji wajibu wa kurejeshwaj wa maji kwenye chanzo cha maji yalikochukuliwa baada ya kuyatumia na kuhakikisha kuwa maji yaliyorejeshwa kwenye chanzo chochote kilichoelezwa hayakuchafuliwa.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa