Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Juma Zuberi Homera leo amezindua rasmi safari za meli ya Mv.Mbeya II ambazo zilisimama kwa muda wa miezi tisa kufuatia hitilafu iliyojitokeza baada ya kupata dhoroba ikiwa inakaribia kutia nanga katika Bandari ndogo ya Itungi iliyopo Kyela.
Meli hiyo ilisimama kutoa huduma kutokana na hitilafu iliyotokea wakati wa dhoruba mnamo Mei 3, 2021 ikiwa kwenye safari zake za usafirishaji na hivyo ilipelekwa kwenye chelezo (Floating Dock) kwa ajili ya matengenezo.
Hata hivyo baada ya matengenezo kukamilika, ilifanyiwa ukaguzi na taasisi ya Udhibiti wa vyombo vya maji (TASAC) ambapo Meli hiyo ilipewa cheti kwa ajili ya kuendelea kufanya shughuli zake za usafirishaji.
Akizungumza na Abiria pamoja na watumishi mbalimbali wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA kabla ya Meli hiyo kuondoka Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mh Juma Zuberi Homera ameishukuru Serikali chini ya uwongozi wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuweza kufanikisha matengezo ya Meli hiyo ambayo ni msaada mkubwa kwa wananchi katika kurahisisha safari zao na kusafirisha mizigo yao.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa