Serikali Mkoani Mbeya imewahamisha wananfunzi 86 wa kidato cha kwanza waliokuwa wanasoma shule ya Sekondari ya Mkola Kata ya Makongorosi kwenda shule ya Matundasi kuanzia tarehe 23 Aprili, 2018 baada ya kuridhishwa na kukamilika kwa ujenzi wa shule hiyo kupitia nguvu za wananchi
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla jana alipokuwa anakagua sekondari hiyo baada ya kupokea malalamiko mengi ya wazazina wananchi wa Kata ya Matundasi kutokana na kutofunguliwa shule hiyo.
Alisema amelazimika kufika kujiridhisha na ujenzi na kwamba akiwa kama kiongozi ni jukumu lake kufanya maamuzi magumu ili kujenga mahusiano mazuri baini ya Serikali na wananchi.
"Nimefika kujiridhisha kimsingi mnyonge mnyongeni haki yake mpeni kwa kweli mmefanya kitu kizuri sana sasa kikubwa muendelee kuchangia ili kuongeza idadi ya vyumba vya madarasa ili viweze kukithi mahitaji
kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne"alisema.
Diwani wa kata ya Matundasi Bw Kimo Choga (CCM) alisema kwa kipindi cha miaka nane sasa tangu shule hiyo ikamilike wamekuwa wakifuatilia wilayani kuomba ifunguliwe ambapo wamekuwa wakielezwa sababu zisizo za msingi jambo ambalo lilikuwa likiwakatisha tamaa wananchi.
Mhe Diwani amemwambia Mkuu wa Mkoa kuwa ujenzi ulikamilika mwaka 2011 ambapo mpaka sasa ni miaka 8 haijafunguliwa na kuomba ujio wake uwe chachu ya kutokomeza siasa inayoletwa na Viongozi wa wilaya hiyo.
Choga amesema kuwa kutaondokana na changamoto ya kutembea umbali mrefu wa kilometa 25 kufuata elimu na kuwasogezea uwezo kupata elimu kwa karibu bora itakayozalisha wasomi wa kizazi kijacho.
Mkaguzi mkuu na mthibiti wa ubora wa shule Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Merchant Mtandika, alisema shule hiyo imekidhi vigezo vinavyohitajika na kwamba kwa sasa atashughulikia usajili wakati wanafunzi wakiendelea na masomo.
Mkazi wa Matundasi Mariam Gabriel alipongeza maamuzi ya Mkoa kwani kama wananchi walishangazwa kwa kutofunguliwa kwa shule hiyo ambao imekidhi vigezo kama miundombinu ya vyumba vya madarasa,maabara ya kisasa,matundu ya vyoo jengo la utawala na ofisi za walimu.
Awali April 11 mwaka huu wanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Mkola waligoma kuendelea na masomo wakishinikiza serikali ya wilaya kufungua shule ya kata ya Matundasi ili kuwaondoka katika
changamoto ya kutembea umbali mrefu kufuata elimu
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa