Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Juma Zuberi Homera leo 31/05/2022 ameshiriki kongamano la kuliombea Taifa na kumuombea Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan na kumpongeza kwa uongozi bora ambao anaendelea kuufanya nchini. Kongamano hilo ambalo liliongozwa na viongozi mbalimbali wa dini kutoka nchini Tanzania ambao waliongoza maombi ya kuliombea Taifa amani na mshikamano limefanyika katika Jiji la Mbeya.
Homera amesema anatambua mchango mkubwa unaofanywa na viongozi wa dini nchini Tanzania kwa madhehebu yote, na kwamba serikali itaendelea kuungana nao na kushirikiana ili kuhakikisha Taifa hili linakuwa na Amani na Upendo bila ya ubaguzi.
“Nawashukuru viongozi wa Dini kwa jambo mlilolifanya kwa kutambua mchango mkubwa anaoufanya Mh. Rais kwa muda huu mfupi aliokaa madarakani katika nchi hii kwa kuandaa kongamano hili la kumuombea na kuliombea taifa kuwa na amani mkitambua mchango wake na kuendelea kumtia moyo kwa kuwa changamoto ni nyingi lakini bado anaendelea kupambana nazo ili kuleta maendeo” alisemaHomera.
Mkoa wa Mbeya unaendelea kuungana na viongozi wa dini Nchi nzima katika kuhakikisha taifa linakuwa na upendo na amani.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa