Serikali imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 1.7 kwaajili ya Ujenzi na ukarabati wa Vituo vya Afya vitatu katika Kata za Ilembo, Santilya na Ikukwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Mganga Mkuu wa Wilaya Dk Lausi Chomboka ameyasema hayo alipokuwa akitoa Taarifa ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kituo cha afya cha Ilembo katika ziara ya Mkuu wa Mkoa kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho.
Dk Chomboka amesema kuwa fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa Maabara, Jengo la Upasuaji, wodi ya wazazi, wodi ya watoto, nyumba ya mtumishi, chumba cha kuhifadhia maiti, mfumo wa kukusanyia maji na sehemu ya kuchomea taka.
Amesema kuwa mradi wa ujenzi wa kituo cha afya Ilembo unagharimu Kiasi cha shilingi milioni 400 na ituo hicho cha afya kitahudumia vijiji 10 vyenye wakazi 17,166 kati hao, Wanawake 9,278 na wanaume 8,888 na kwamba Idadi ya wananwake wenye uwezo wa kushika mimba ni 3,777.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amesema kuwa amekuja kujiridhisha namna Halmashauri na wananchi walivyojipanga kutumia fedha hizo zilizoletwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya
Mhe Makalla amewataka wananchi kushirika katika ujenzi wa kituo hicho mpaka kitakapokamilika bila kujali itikadi za siasa kwa kuwa wanatakaotumia kituo hicho ni watu wote wa kata hiyo na amewaonya wanaopita kwa wananchi kuwashawishi kutoshiriki katika shughuli za miradi ya maendeleo.
Mhe Makalla ameagiza watumishi wa afya katika halmashauri na ofisi ya mkoa kuelekeza nguvu ya utendaji kazi katika ujenzi wa kituo cha afya Ilembo na ifikapo Mei 30 mradi ukamilike.
"Kuna watu wamekaa tu maofisini sasa ninaagiza kuanzia sasa waweke kambi huku ilembo ili kusukuma kasi ya ujenzi wa mradi huo na ujengwe kwa ubora wa hali ya juu ili jamii iweze kupata huduma bora za afya ya Msingi hususani upasuaji na kuacha kutembea umbali mrefu kufuata huduama za afya,” amesema
Naye Kaimu Mganga Mkuu, Dk.Yahya Msuya amesema katika mpango wa awamu ya kwanza ya utekelezaji wa ujenzi na ukarabati wa vituo vya afya,kati ya vituo 44 katika halmashauri 82, Mkoa wa Mbeya ulipata Vituo viwili katika Halmashauri ya Rungwe Kituo cha Afya Ikuti na Halmashauri ya Kyela Kituo cha Afya Ipinda.
" Kutokana na kufanya vizuri katika ujenzi wa vituo vya afya Rungwe na Kyela katika awamu ya pili kati ya vituo vya afya 139 nchi nzima mkoa wa mbeya umepata vituo sita na katika hatua za awali tumeanza na vituo vya afya Ikukwa,Santilya na Ilembo ambavyo vitagharimu Sh bilioni 1.7,"amesema.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa