Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi ya Vijiji ni moja ya mipango mkakati ya utekelezaji utakaohakikisha wakulima wadongo na wafugaji wananufaika na sera ya uwekezaji kati ukuaji wa maaendeleo ya uchumi nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mipango Miji Bw Geoffrey Mwanjobele wakati utoajia elimu wa kujenga ujirani mwema kati ya wananchi na hifadhi na kuwashauri wafugaji kutenga maeneo kwaajili ya malisho ya mifugo
Bw. Mwanjobele amesema kuwa Serikali ya kijiji kupitia kamati ya upangaji wa matumizi bora ya ardhi Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali yatakiwa kuhakikisha inatenga maeneo ya malisho ya mifugo ili kuondokana na tabia ya wananchi kupeleka mifugo yao ndani ya maeneo ya hifadhi.
" Kuna kitu hakijakaa sawa kwetu sisi wafugaji, sisi ni wafugaji na wakulima lakini tunakumbuka kutenga eneo la kilimo na kusahau kutenga eneo kwaajili ya malisho ya mifugo yako".
Afisa Tawala wa Wilaya Bibi Oliver Sulle ameiambia Serikali ya kijiji kuwa ndio wenye mamlaka ya kupanga na kubadili matumizi bora ya ardhi ni kijiji na kuwataka wafugaji kuhudhuria mikutano ya Vijiji ili waweze kutetea kupata maeneo yao.
Naye Jafari Mangula mwanakijiji wa Mapogoro Kata ya Mapogoro ameiomba Serikali kuongeza maeneo ya malisho kwa sababu mifugo imekuwa mingi sana
Elimu hiyo imetolewa na Wataalamu kutoka taasisi za TANAPA, TAWA, TFS, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa