Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Dkt Tulia Ackson ametoa msaada wa saruji mifuko 100 na mabati 100 katika Shule ya Sekondari Pankumbi Halmashauri ya Jiji la Mbeya vyenye thamani ya sh. Milioni 3.9.
Msaada huo ulikabidhiwa jana nkwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla katika halfa fupi iliyofanyika shule ya Sekondari Pankumbi na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mkoa wa Mbeya.
Dkt. Tulia amesema msaada huo umetolewa kupitia Wadau mbalimbali wa maendeleo kushirikiana na Taasisi ya Tulia Trust na kwamba lengo ni kusaidiana na Serikali katika kuboresha huduma muhimu hususani Elimu na afya.
"Tulia Trust iko bega kwa bega na Serikali katika kuhakikisha inaboresha huduma muhimu katika jamii, kwa kushirikiana na mdau mkubwa wa maendeleo Mkoa Ndele Mwaselela."amesema.
Aidha, amepongeza jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwa kujiwekea utaratibu wa kusimamia na kutekeleza kwa vitendo shughuli za miradi ya maendeleo na kwamba kusema huo ndo uzalendo unaohitajika katika Taifa la Tanzania.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla ameuagiza Uongozi wa Shule hiyo pamoja na Diwani wa Kata kuhakikisha misaada hiyo iliyotolewa inatumika kwa wakati na si kuigeuza miradi ya watu wachache.
“ Ninajua kuna baadhi ya watu misaada inapotolewa kwa ajili ya maendeleo wanaweka na kuifungia majumbani kwao. Sitaki kusikia hilo jambo linatokea katika shule hii nitarudi tena kuja kukagua kama ujenzi huo umefikia katika hatua gani “amesema
Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Sister Seken ,alisema wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa, uhaba wa vyumba vya madarasa na thamani za ofisi za walimu jambo linalowalizimu kutumia madawati ya
wanafunzi.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa