Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila ametangaza kuipa jina la Chifu Rocket Mwanshinga(Chief Rocket Mwanshinga Pre& Primary English Medium School) Shule ya Awali na Msingi ya Mchepuo wa Kiingereza iliyopo Kata ya Nsalaga Halmashauri ya Jiji la Mbeya
Mhe Chalamila ameyasema hayo leo Nsalaga alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo na kusema kuwa lengo la kutoa jina la Shule kwa Chifu Mwanshinga ni kutambua mchango wake katika ujenzi wa shule hiyo.
Chalamila amesema ujenzi wa shule hii ya Serikali ya Mchepuko wa kiingereza ni katika kuunga vipaumbele vya serikali katika elimu kwa kupeleka huduma karibu na wananchi ili waweze kuwapeleka watoto wao shule zilizo karbu na maeneo wananyoishi.
“Mhe Rais Mama Samia Suluhu ameingia madarakani wala kipaumbele chake sio kuhamasisha wizi katika Taifa, kipaumbele chake ni kuhakikisha tunapeleka huduma kwa watanzania, kuhakikisha tunafanya miradi inayoendana na fedha inayotolewa na kuhakikisha wananchi wanaona kodi zao zinavyotumika” Mhe Chalamila
Akisoma taarifa ya ujenzi wa shule hiyo Mwl Janet wa shule hii umetokana na uhitaji mkubwa wa shule ya mchepuo wa kiingereza kwa wakazi wa Uyole na maeneo ya jirani, na shule imekwisha sajiliwa kwa nambaEM.18629
“ Shule hii tunatarajia kusajili wanafunzi 270, Awamu ya kwanza ujenzi huu ni wa vyumba sita vya madarasa, jingo la utawala na matundu kumi na sita ya vyoo vya wanafunzi ambapo matundu nane ni kwa ajili ya wasichana na matundu nane ni kwa ajili ya wavulana” Mwl Janet
Naye Chifu Mwanshinga ameishukuru Serikali ya Mkoa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa kuona umuhimu wa kuipa shule hiyo jina lake na kuahidikutoa ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha shule hiyo inakamilika kwa wakati ili watoto waanze kusoma
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa