Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe. Beno Malisa amewakumbusha Maafisa Manunuzi wa idara ya afya kusimamia vema fedha za Serikali wakati wa Manunuzi.
Akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, kwenye kufunga Semina ya siku tano ya Manunuzi kwa Umma ilyojumuisha Maafisa Manunuzi, wakaguzi wa ndani na Maafisa masuhuri wa Sekta ya Afya Nchini iliyofanyika katika Chuo cha TIA Mbeya Iliyojumuisha washiriki 56 ambapo wamejifunza sheria ya manunuzi namna ya kuandaa mikataba taratibu za Manunuzi.
Aidh Mh.Beno amesema kuwa Kwa mafunzo hayo yatakwenda kuleta matokeo chanya upande wa Manunuzi kwa kusimamia vyema Mikataba yenye tija na wazabuni wanaoweza kutimiza wajibu wao.
Annacreta Rugwaumo Mkaguzi wa ndani Hospital ya Rufaa Temeke ameahidi kwenda kuwa muadilifu na kuwashauri watendaji pale wanapokuwa wamekwenda kinyume na taratibu za Manunuzi.
Naye Dkt. Joseph Kimaro Mganga mfawidhi Hospital ya Rufaa Temeke amesema Semina hiyo itawasaidia kuindoa utendaji wa mazoea kwa kufanya Manunuzi yenye tija kwa kuhakikisha kwamba vifaa tiba na dawa zinapatikana.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa