Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila amezitaka taasisi za dini kuchagua viongozi waadilifu na walio werevu ili waweze kusimamia miradi ya maendeleo ya taasisi zao kikamilifu.
Mhe. Chalamila ameongea hayo leo alipokutana na viongozi wa dini mbalimbali kwa leongo la kujitambulisha na kuwataka kusimamia miradi yao kwa ukamilifu kwa kuwa inakuza uchumi wa mkoa.
Amesema kuwa taasisi za kidini zina mchango mkubwa sana katika masuala ya afya, Elimu, maadili na ajira hivyo zikikosa usimamizi mzuri miradi hviongozi wanajimilikisha miradi hiyo kama ya watu binafsi.
“ Kuna baadhi ya vyo Mbeya vimefungiwa udahili wa wananfunzi kwa miaka miwili sasa na hili linapelekea kudidimiza hali ya uchumi wa kuanzia ngazi ya Serikali hadi ngazi ya familia.” Mhe Chalamila
Chalamila amesema kuwa taasisi hizo zina jukumu la kuendelea kuhubiri na kuomba kwa Mwenyezi Mungu kupata viongozi walio bora na kuwataka kutumia waumini wao kupata kazi Serikalini.
Aidha, ameziomba taasisi hizo kuendelea kuuombea mkoa kuondokana na suala la ubakaji wa watoto ambao umekithiri kutokana na imani za kishirikina hasa katika Wilaya ya Chunya na Mbeya.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa