WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Suleiman Jaffo amewaonya Mameneja na Wanasheria wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini(TARURA) nchini kuacha kufanya kazi kwa mazoea badala yake wazingatie maadili ya kazi waliyopewa.
Mhe.Jaffo ametoa agizo hilo leo jijini Mbeya,alipofunguaSemina ya Siku tano ya Watendaji wa Tarura kutoka mikoa saba iliyopo Kanda ya nyanda za juu kusini.
Ameitaja Rushwa kuwa miongoni mwa mambo makubwa ambayo yamekuwa yakisababisha Zabuni nyingi kutotekelezwa kwa kufuata mikataba na kuisababishia hasara Serikali.
Amewataja wanasheria wa Serikali kuchangia kuipa Hasara Serikali kwa kushindwa kusimamia Sheria hususani kesi za wazabuni zinazopelekwa mahakamani hatua aliyosema inatokana na wau wa kada hiyo kula sahani moja na wakandarasi.
Amesema wakandarasi wengi wamekuwa wakishindwa kutekeleza kazi kwa mujibu wa mkataba na kuzusha mivutano ambayo mwishowe hufikia hatua ya kufungua kesi mahakamani lakini ajabu ni kuwa Serikali imekuwa ikishindwa kesi hizo na kulazimika kuingia hasara kwa kulipa fidia.
Waziri huyo pia amewataka mameneja wa Tarura kutambua kuwa yeyote atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake atambue kuwa hatoweza kufika mwezi wa saba mwaka huu akiwa kwenye nafasi hiyo.
Amesema Tarura inategemewa na Taifa katika kuleta mabadiliko makubwa hasa katika kuelekea uchumi wa kati unaotegemea viwanda ambapo hauwezi kufikiwa pasipo uwepo wa miundombinu ya barabara iliyo bora.
Amesisitiza kuwa miundombinu bora itawaondolea wakulima adha ya kusafirisha mazao kutoka mashambani hadi yaliko masoko hivyo kurahisisha upatikanaji wa malighafi za viwanda
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla ameahidi kuendelea kusimamia kwa karibu miradi yote itakayotekelezwa na wakala huo huku akisisitiza kuwa hakuna atakaeachwa salama iwapo atabaini matumizi mabovu ya fedha za umma.
Mhe. Makalla amesema wananchi hususani wa maeneo ya pembezoni wana matarajio makubwa na Tarura hali inyotokana na adha iliyowakabili kwa miaka mingi ya ukosefu wa miundombinu rafiki ya barabara.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa