Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amekabidhiwa majengo ya na Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa na kuzindua kuanza kutumika kwa majengo hayo kwa ajili ya chuo cha VETA katika Halmashauri ya Busokelo Wilayani Rungwe
Akiongea katika uzinduzi huo Mhe. Makalla amewashukuru Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa (TANAPA) kwa kuchangia ujenzi wa kituo cha kulea watoto Yatima ambacho kimebadilishwa matumizi na kutumia majengo hayo kwa ajili ya Chuo cha Ufundi VETA.
Mhe. Makalla amemshukuru aliyekuwa Mbunge wa Busokelo Pro. Mark Mwandosya kwa kuasisi ujenzi wa kujenga majengo hayo na kuwataka wananchi wa Busokelo kutunza majengo na kuwataka Viongozi wa Wilaya na Halmashauri kukisimamia na kukitunza ya chuo hicho.
Aidha, Mkuu wa Mkoa amewataka vijana waliomaliza darasa la saba, kidato cha nne na sita kujiunga na chuo hicho kwa kozi za ufundi wa aina mbalimbali kwa ajili ya kuweza kujiari na kuajiriwa baada ya kuhitimu mafunzo hayo ya ufundi katika chuo hicho.
Chuo cha VETA Busokelo kimeanza mafunzo rasmi mwezi wa tatu mwaka huu ambapo mpaka sasa wanafunzi 69 wamesajiliwa kwenye kozi mbalimbali za chuo hicho.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa