Faida zinazopatikana kutokana na uhifadhi zinarudi kwa wananchi kupitia shughuli za maendelo – Lihiru
Hayo yamesemwa na mjumbe wa timu maalumu ya kutoa elimu ya uhifadhi na ujirani mwema Mhifadhi kutoka Hifadhi ya Taifa kitulo Ndg. Agricola Lihiru alipokuwa akitoa elimu kuhusina na uhifadhi wa hifadhi za taifa pamoja na ujirani mwema siku ya tarehe 12/03/2020
Lihiru amesema kwamba zipo faida nyingi tunazoweza kuzipata kutoka kwenye uhifadhi ikiwemo kuendeleza miradi ya maendeleo iliyoibuliwa na wananchi kwa kuchangia asilimia 90 ya mradi na kuchangia kwenye mfuko wa taifa ili kusaidia shughuli za kimaendeleo.
Mhifadhi amebainisha baadhi ya miradi iliyofadhiliwa na Hifadhi ya Taifa za Tanzania (TANAPA) kuwa ni pamoja na ujenzi wa bwalo la shule ya sekondari ya Mawindi, utengenezaji wa madawati katika shule ya msingi ya Luango, ujenzi wa vyumba vya madarasa Kata ya Igava pamoja na ujenzi wa zahanati ya Madibira.
Naye Afisa Ujirani Mwema kutoka Hifadhi ya Taifa ya Kitulo Ndg Mollel Heriel ameweza kubainisha mambo mbalimbali ambayo hayaruhusiwi katika maeneo ya hifadhi kuwa ni pamoja na kutokufanya shughuli za kibinadamu kama kuwinda , kuingiza mifugo, kuweka makazi, kuchoma moto na mkaa kuwinda wanyama pori, kuvuna misitu,, uvuvi, kuwinda , kuchimba madini na kuingia na silaha yoyote.
Aliongeza kuwa muingiliano wa wanyama wa kufugwa na wanyamapori inaharibu uasilia wa wanyama pori pamoja na muingiliano wa magonja kutoka kwa wanyama wa kufungwa kwenda kwa wanyama pori au wanyama pori kwenda kwa wanyama wa kufugwa majumbani
Muikolojia Kutoka Hifadhi ya Taifa Ruaha Ndg Daniel Mathayo aliongeza kuwa kuna hifadhi 22 za taifa kwa sasa ambazo zinahifadhi wanyama pori na mazingira ambapo katika hifadhi hizo wananchi na wageni wanaruhusiwa kwenda kufanya utalii wa picha ambapo kwa mtanzania mtu mzima ni tsh. 5000 na mtoto ni 2000 vilevile inaruhusiwa kwenda kufanya matambiko kwa kibali maalumu ili waweze kupatiwa ulinzi.
Aliongeza kuwa TANAPA imeanzisha tuzo ya uhifadhi mazingira ambayo inashindanisha wananchi ambao wanafanya shughuli za uhifadhi wa mazingira kama watu binafsi, taasisi, vikundi na jumuiya za watumia maji ili kuimbarisha ujirani mwema, kuboresha mazingira na vyanzo vya maji, ambapo kwa sasa imeshafanyika kwa wilaya za Mbarali, Wangingombe, Makete, Mufindi na Kilolo na mwaka huu imeongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya.
MWISHO
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa