Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amewataka Wakala wa Barabara (TANROADS) kuchukua hatua za dharura kwa kuanza kujenga barabara nyingine ya mchepuko Mbalizi kwa ajili ya magari ya mizigo yanayoenda nje ya nchi.
Mhe Makalla ameyasema hayo leo alipotembelea eneo la Mlima wa Iwambi ilipotokea ajali ya magari matatu na kusababisha vifo vya watu ishirini na majeruhi 48.
Amesema kuwa ni wakati Mkoa unasubiria kutekeleza mpango wa serikali wa kujenga barabara kubwa ya mchepuko kutoka Uyole hadi Songwe hatua za dharua zichukuliwe kuondoa magari hayo kupita eneo la Mlima Iwambi.
Aidha, Mhe Makalla ametoa pole kwa wananchi wote waliopoteza ndugu zao katika ajali hiyo na kuwatakia afya njema majeruhi wote wa ajali hiyo
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Musa Taibu Chanzo cha ajali ni roli la mizigo kukata breki na kugonga mabasi madogo matatu ya kubeba abiria mawili yaliyokuwa yakitoka Mbalizi kwenda Mwanjelwa na moja lililokuwa likielekea mjini Mbalizi.
Amesema majeruhi wa ajali hiyo wamekimbizwa katika Hospitali Teule ya Ifisi Mbalizi na katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi huku akiwataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Hata hivyo kufanikiwa kwa shughuli za uokoaji wa miili ya marehemu na majeruhi ni kufuatia ushirikiano wa Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi JWTZ.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa