Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde: Juma Z. Homera amekutana na Balozi wa Norway nchini Tanzania Mh: Tone Tinnes Leo Septemba 25 2024 na Kujadiliana fursa mbali mbali hasa Namna ya kuimarisha Kilimo Cha Mpunga/Mchele Wilayani Mbarali zao la Parachichi, Pareto Mafuta ya Kula n.k
RC Homera amesisitiza Maeneo mahususi ya Kuimarisha Mahusiano mbali na Kilimo ni Uwekezaji wa Viwanda Vikubwa vya kuchakata Mazao ya Parachichi na Kakao, Teknolojia Bora na Rafiki hasa Taasisi za Utafiti wa Kilimo Mbeya(TARI) na MATI Igurusi na MATI Uyole.
Aidha amemuomba Balozi Tinnes kukubali Ombi lake la kuunganisha Mahusiano ya Majiji Mawili(Mbeya) na Jiji mojawapo nchini Norway kwa Lengo la kukomaza Mahusiano ya Kibiashara za Kimataifa Kati ya Tanzania na Norway katika Sekta Kadha wa kadha.
Kwa Upande wake Balozi Tone Tinnes baada ya kumsikiliza RC Homera ameishukuru Tanzania kwa Mahusiano Mema yaliyopo na Nchi yake na ameahidi kuendeleza Mashirikiano hasa katika Uwekezaji wa sekta zote zinazopatikana nchini hasa Mbeya.
Hata hivyo ameitakia Kheri Tanzania Kelekea kwenye Zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa linalotarajiwa Kufanyika Mwezi Novemba 2024.
Balozi Yuko Mkoani Mbeya Kwa Ziara ya Kikazi ya Siku Mbili na Leo Yuko Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa