Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe alipokuwa anafungua kikao cha Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kilichofanyika katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya.
“Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizosaini makubaliano ya kufanya biashara bila mipaka barani Afrika na kwamba tangu kusainiwa kwa mkataba huo Watanzania wanaruhusiwa kufanya biashara zao ndani na nje ya mipaka ya Nchi.” Alisema Kigahe.
Mhe. Kigahe aliwashauri viongozi hao kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji kupitia fursa mbalimbali zilizopo katika Mikoa hiyo kama vile bandari za Itunge, Kiwira, Kasanga na Kalema ambazo zinatumika na wafanyabiashara wa ndani na nje kusafirisha bidhaa zao.
Pia, Mwenyekiti wa Wakuu wa Mikoa Nyanda za juu ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mhe. Juma Homera alisema kikao hicho kina tija katika kuleta maendeleo kwa wananchi kupitia fursa mbalimbali za kibiashara na kilimo ili kuwakwamua wananchi katika wimbi la umasikini kwa kunufaika na uwekezaji kupitia mipaka mbalimbali ya nchi.
“Ushirikiano wa kibiashara katika mataifa mbalimbali sio mzuri na kikao hiki ni muhimu kujadili mambo ya kufanya ili kuwezesha Wananchi kufanya shughuli zao bila tatizo lolote ukilinganisha na ilivyo sasa ambapo bado kuna tatizo”. Alisema Homera
Wakuu wa Mikoa nane na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, wameshiriki katika kikao cha ujirani mwema jijini Mbeya kujadili namna ya kuondoa vikwazo vya kibiashara baina ya Tanzania na mataifa jirani pamoja na ulinzi wa mipaka ya nchi ikiwemo Mbeya ambayo ndio mwenyeji, Songwe, Rukwa, Njombe, Iringa, Ruvuma, Katavi pamoja na Tabora ambayo walikuwa wageni waalikwa.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa