Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila, ameshauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuangalia uwezekano wa uwepo kwa mfumo wa mtaalamu wa utoaji elimu ya mlipa kodi kuanzia elimu ya sekondari na vyuo vikuu nchini ili kuwezesha taifa kuwa na wazalendo wataojua umuhimu wa kulipa kodi.
Chalamila alisema jana wakati akizunguzma na uongozi wa TRA, Makao makuu na mkoa wa Mbeya kufautia kuanza kwa zoezi la utoaji Elimu ya mlipakodi, mlango kwa mlango, duka kwa duka iliyoanza katika baadhi ya wilaya Mkoani hapa.
Alisema uwepo wa mtaala huo utasaidia kuzalisha vijana wazalendo ambao watakuwa mstari wa mbele kulipa mapato serikali kulingana na shughuli mbalimbali za kiuchumi na hivyo kuchochea ukuaji wa miradi ya maendeleo hususan barabarani na taifa kupiga hatua kutokana na kodi za wananchi.
"Mkoa wa Mbeya wafanyabiashara wana kasumba ya kukwepa kukipa kodi pamoja na matumizi ya Efds sasa ili kufanikiwa washirikisheni madiwani wakati wa kutoa Elimu ili wawasikishe kwenye vikao vya mabaraza ya madiwani jambo ambalo ltawasaidia kufikia malengo kwa Elimu kuwafikia wananchi na kulipa kodi kwa hiari "alisema.
Alisema kwa kuwa wanaanzia kutoa elimu wilayani Chunya pia kuna changamoto ya utoshaji wa Madini hususani maeneo ya machombo ambayo hayajasajiliwa jambo ambalo pia linachangia upotevu wa mapato hivyo ni jukumu lenu Tra kuliangalia wakati wa utoaji Elimu Ya mlipa kodi.
Afisa kodi Mkuu, Elimu kwa mlipa kodi Makao makuu, James Ntalika alisema kuwa wazo la kuanza kwa mtaala ataliwasilisha makao makuu kwani ni jambo jema ambalo litachochea ulipaji kodi kwa hiari.
Alisema uwa zoezi la utoaji elimu linaendelea nchi nzima kwa Mkoa wa Mbeya walianzia wilayani chunya lengo ni kuwapatia Elimu wananchi hususan wafanyabishara kujua umuhimu wa kulipa kodi na matumizi ya Efds.
Meneja wa Tra mkoa wa Mbeya, Eunice Liheluka aliwataka wafanyabishara kutoa ushirikiano kwa maofisa wanaowawafikia na si kufunga maduka na kukimbia kwani serikali ina malengo mazuri katika kuhakikisa wanalipa kodi kwa wakati na si kukwepa.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa