Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila ameitaka Mamlaka ya Mapato Mkoa wa Mbeya (TRA) kuendelea kuwabaini wakwepa kodi na wafanyabiashara wasio na nyaraka maalumu za mamlaka hiyo.
Mhe. Chalamila ameyasema hayo leo Novemba 11, 2020 alipokuwa akiongea na wafanyakazi wa TRA Mbeya katika ofisi zao na kuwataka watumishi hao kutotafuta kupendwa katika kazi yao hasa kwa kuwa wanafanya kazi katika ofisi nyeti
“Mhe Chalamila amesema kuwa atakabidhi majina sita ya wafanyabiashara wanaokwepa kodi kwa kujihusisha na ukopeshaji wa fedha kwa wananchi kinyume cha utaratibu na hawana nyaraka zozote kutoka TRA.
"Nimejiridhisha kwa kufanya ufuatiliaji kwani wanakopesha mpaka mamilioni ya shilingi kwa wananchi na wanapokwama kulipa wanawanyanyasa kwa kushika mali zao," amesema.
Amesema akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya Mkoa anahitaji TRA ifanye kazi yake kwa kuhakikisha wanakamatwa na kuchukuliwa hatua kwa kuwa ni miongoni kwa wakwepa kodi na wahujumu uchumi.
Meneja wa TRA Mkoa, Eunice Liheruka amesema atafuatilia suala hilo na kuhakikisha wanabainika kwa kuwa kitendo hicho ni ukiukwaji wa sheria za nchi.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa