Mkuu wa Mkoa wa Mbeya amewataka wafanyabiashara wakubwa kutumia meli za mizigo za MV Njombe na MV Ruvuma kusafirishia mizigo yao ili waweze kufanikisha kufungua fursa za kiuchumi na fursa za kimapato kwa wafanyabiashara pembezoni mwa Bandari ya Itungi na wa Tanzania na Malawi.
Hayo yamebainishwa na Mhe Amos Makalla Mkuu wa Mkoa wa Mbeya wakati alipofanya ukaguzi wa utengenezaji wa Meli mpya ya Abiria na kukagua utendaji wa meli za mbili za mizigo katika Bandari ya Itungi Wilayani Kyela.
Mhe. Makalla amesema kuwa baada ya Kukamilika kwa Meli mbili za mizigo kunasaidia usambazaji wa bidhaa mbalimbali ambazo viwanda vilivyopo Mbeya Aidha, mradi huu utaunganisha Tanzania na Malawi ambapo nchi ya Malawi inategemea sana usafiri wa Meli kwa ajili ya kusafirishia bidhaa za kutoka na kuingia nchi hiyo.
“ Mahitaji na matumizi ya wananchi ni makubwa mno na Serikali ya Mkoa inataka kuona utengenezaji wa Meli hizi unakamilika kwa wakati ili wananchi waanze kunufaika mapema na jitihada za Serikali yao”. Mhe Makalla
Kwa upande wake Meneja wa Bandari Kyela Bw. Ajuaye Msese amesema kuwa mradi wa ujenzi wa Meli Bandari ya Itungi ulikuwa unahusisha meli mbili za mizigo na meli moja ya abiria ambapo meli mbili za mizigo zimeshakamilika na kuanza shughuli za usafirishaji
Bw. Msese amesema kuwa mamlaka imelenga kuifanya Bandari ya Itungi kuhudumia abiria na Mizigo mchanganyiko na ile ya Kiwira kuhudumia Mizigo kama Makaa ya Mawe, Mbolea na Saruji kama sehemu ya utekelezaji wa sheria ya Mazingira.
Bw. Msese amesema kuwa Mamlaka iko katika hatua nzuri za kuhakikisha inapata eneo katika Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya ujenzi wa Bandari Kavu ambayo itakuwa kiungo muhimu kwa Mizigo inayosafirishwa kutoka Dar es Salaam kupitia reli ya TAZARA kwenda nchi jirani Malawi, Zambia na DRC
Mhandisi Mkuu Bw. Khalid Songoro amesema kuwa meli ya abiria imekamilika asilimia 60 ya kazi na kuchelewa kumaliza utengenezaji huo ni kutokana na ufinyu wa nafasi bandarini na kupungua kwa kina cha maji.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa