Naibu Balozi wa Netherland nchini Bi Lianne Houben ameahidi kuwa nchi yake imekusudia kukuza kilimo na biashara ya zao la viazi Mkoani Mbeya.
Bi Houben ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla.
Amesema kuwa Kupitia shirika la Maendeleo la Nerthaerland wameuchagua Mkoa wa Mbeya kuendeleza zao hilo kwa kuhamasisha, elimu kwa wakulima na zana za kilimo ili zao hilo lilimwe kwa wingi na wafanyabiashara wa Nertherland wafanye biashara na wakulima hao.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla amepokea kwa furaha mipango hiyo mizuri na kusema kuwa Serikali ya Mkoa itahakikisha fursa hiyo haipotei
Aidha, Mhe Makalla amesema kuwa kukamilika kwa Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Songwe itatoa fursa zaidi ya usafirishaji wa viazi nje ya nchi kwani uwanja huo utakuwa na uwezo wa kupokea Ndege za mizigo ya tani 500.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa