Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla ameiagiza Halmashauri ya Jiji la Mbeya kuanza kusambaza vifusi katika barabara iliyopo Mtaa wa Mkombozi Kata ya Ruanda kabla mvua hazijaanza kunyesha ili kuondoka kero kwa wananchi wa Mtaa huo.
Akizungumza katika ziara yake ya kukagua barabara za Halmashauri ya Jiji Mhe. Makalla amesema kuwa Halmashauri ya Jiji ichukulie ukarabati wa barabara hiyo kama kazi ya dharua nakuingiza katika vikao vya Baraza la Madiwani kuweza kuidhinisha ili kuwasaidia wananchi wa Mtaa huo.
Wakiongea na Mkuu wa Mkoa Wananchi wa Mtaa huo wameuomba uongozi wa Halmashauri ya Jiji kuendelea kusambaza vifusi vilivyomwagwa katika barabara ya mtaa huo ili visisababishe maji kuingia kwenye nyumba zao. Aidha wananchi hao walishauri kuwa kuwepo kwa makaravati mengi katika barabara hiyo ili kuwezesha maji kupita kirahisi katika mitaro ya maji.
Naye Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ alisema kuwa amepata malalamiko mengi ya Wananchi wa eneo hilo wakati yuko bungeni wakilalamikia barabara hiyo na kuona umuhimu wa kuongozana na Mkuu wa Mkoa katika ziara hiyo.
Aidha, Mhe. Mbilinyi alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kushughulikia kero za wananchi kwa kwenda katika maeneo yenye matatizo ili na yeye ajionee na kuwasikiliza kisha kufanya maamuz
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa