Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe.Albert Chalamila amesema moja ya vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kwamba wananchi hasa wa sekta zisizo rasmi wanapata matibabu kupitia mifumo ya bima ili kufikia lengo la afya bora kwa wote.
Mhe. Chalamila ameyasema hayo leo wakati akifanya uzinduzi wa usajili wa wanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii Uliyoboreshwa na kusema serikali ina malengo ya muda mrefu ya kuwa na mfuko moja wa bima ya afya ambao kila mwananchi atachangia.
“Ninaagiza Wakurugenzi kuhakikisha mnaandaa mikataba haraka kwa ajili ya maafisa waandikishaji ngazi ya Vijiji/Mitaa na wasimamizi wa CHF ngazi ya Tarafa. Aidha simamieni zoezi la ununuzi wa simu za vituo vya kutolea huduma”. Mhe Chalamila
Akisoma taarifa Mratibu wa CHF Mkoa Bibi Selina Mtenya ameishukuru Wizara ya OR-TAMISEMI kwa kuwezesha mafunzo ya mfuko wa afya ya jamii iliyoboreshwa katika ngazi ya Mkoa na Wilaya na kuwashukuru wadau wa maendeleo GIZ kwa kuwezesha magunzo ya CHF ngazi ya Tarafa na Vijiji/Mitaa.
Bibi Mtenya amesema kuwa usajili utafanyika kwa Kaya kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya simu ya mkononi (Smartphones) na hakutakuwa na gharama za kupiga picha na kila mwanachama atapatiwa kitambulisho chake. “Kiwango cha mchango wa mfuko wa afya ya jamii ulioboreshwa ni sh.30,000 kwa kaya ya watu sita kwa Mawala na Serikali itachangia kiasi kama hicho cha sh. 30,000 na mwanachama atapata huduma kuanzia ngazi ya za Zahanati, Kituo cha Afya, Hospitali za Wilaya na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa kizingatia utaratibu wa rufaa.” Bibi Mtenya.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji SSP James Kasusura amehidi kufanya hamasa kuanzia ngazi ya mitaa na kuhakikisha wanaandikisha wanachama wengi ili kuuweka mkoa katika nafasi nzuri.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa