Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Albert Chalamila amemtaka mwekezaji wa machimbo ya malulumalu Bw. Michael Simbaulemi kuwa mzalendo kwa kulinda kwa rasilimali ya madini na kuhakikisha wananchi na serikali wanafaika na madini hayo
Mhe. Chalamila ameyasema hayo leo alipotembelea na kukagua machimbo ya malumalu (malble) yaliyopo Kata ya Itawa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya na kumtaka mwekezaji wa machimbo hayo asaidie katika kuimarisha huduma za jamii za eneo hilo.
“Ni faida kubwa kwa madini kama haya kugundulika hapa kwetu na tuamini baada ya muda taifa litapata fedha nyingi kupitia madini hayo ambazo zitasaidia katika kuimarisha miundombinu ya barabara, afya na elimu”. Mhe Chalamila
Naye Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Mbeya Ndugu Sabai Nyansiri amesema kuwa mwekezaji wa machimbo hayo ni mzawa wa na anan leseni ya uchimbaji mdogomdogo kwa masharti ya kufanya kazi na kuajiri wananchi wa vijiji vinavyozunguka machimbo hayo.
Bw. Nyansiri amemtaka mwekezaji huyo kulinda mazingira ya machimbo hayo na kuongeza ukubwa wa mitaro ili mawe yanayochimbwa yasije kuporomoka na kuleta athari kwa wananchi.
Mwekezaji wa Machimbo hayo Bw. Michael Simbaulemi Amesema kuwa tayari ameshachimba mawe sita ambayo yapo tayari kusafirishwa kwenda Brazili pale taratibu na vibali vitakapokuwa tayari kwa sababu bado Serikali haijaruhsu kusafirisha madinin nje ya nchi.
Bw. Simbaulemi amesema ameajiri vijana kutoka vijiji vilivyopo katika maeneo ya machimbo ingawa baadhi ya wananchi hawataki kufanya kazi katika machimbo
Bw. Simbaulemi ameomba ushirkiano kutoka kwa halmashauri kwa kusema kampuni yake bado ni changa sana na mradi wake umeanza mwezi Aprili ,2017
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa