Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Albert Chalamila amewaonya viongozi na wananchi wanaonufaika kwa kuchochoea migogoro katika kijiji cha Ilolo kuacha mara moja na kuwatahadharisha kuwachukulia hatua za kisheria watakaobainika.
Mhe.Mkuu wa Mkoa ameyasema hayo leo Wilayani Rungwe alipokuwa akiongea na wananchi wa Kijiji hicho Kata ya Kiwira alipokwenda kusuluhisha mgogoro wa ardhi kati ya kijiji na Kanisa la Moravian.
Amefafanua kuwa Serikali inataka kuona migogoro inatatuliwa na kuisha na kuwataka viongozi kuwa kitu kimoja ili kutatua vizuri migogoro kwa kutoingiza masuala ya kisiasa katika utatuzi wa migogoro ya wananchi.
“Ukianza kuleta uongo katika kutatua migogoro siwezi kufuga, uwe ni kanisa, Serikali au mwananchi siwezi kufuga. Na katika hili sitamwogopa mtu yeyote yule, tunataka mtatue migogoro iishe na sio kuwa watu wanaochochea migogoro. Naomba mnielewe na niliweke wazi hili” Amesema Chalamila
Mhe Chalamila amewataka wananchi wa kijiji hicho kuwa wanapotaka migogoro ya ardhi kufikia mwisho wasitumie siasa kudai au kuomba kile wanachodhani wanaastahili bali wajenge urafiki na undugu wa kukaa kwa pamoja na Kanisa.
Mhe, Chalamila amewaambia kuwa hakuna mtu atakayesaidia kumaliza migogoro katika kijiji chao zaidi ya wananchi wenyewe wa Ilolo kwa sababu migogoro haiwezi kuisha katika kijiji hicho kutokana na chuki wanazojijengea wenyewe na kuibeba migogoro kiuanaharakati.
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Julius Chalya amekiri kuwepo kwa mgogoro wa ardhi kati ya kanisa la Moravian na Kijiji cha Ilolo ambao ulianza kushughulikiwa Julai, 2017 baada ya wananchi kulalamika kwa Waziri Mkuu kuwa wamenyang’anywa ardhi na kanisa la Moravian ambayo kimipaka ipo ndani ya kijiji cha Ilolo na Syukula.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa