Watumishi wa Umma watakiwa kutokuwa sehemu ya ushabiki wa kisiasa na kupotosha jamii bali wawe mabalozi wazuri wa kutafsiri agenda za serikali katika kutekeleza dhana ya uwajibikaji katika kuleta maendeleo ya taifa na mkoa kwa ujumla.
Hayo yamesemwa na leo na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila wakati akiongea na watumishi wa umma Wilaya ya Mbarali na kusema Serikali haitawavumilia watumishi wanaoingiza itikadi za vyama kwenye utumishi wa umma.
Mhe Chalamila amesema kuwa mtumishi wa umma anaongozwa na kanuni, sheria na taratibu ambavyo vimemnyang’anya uwezo wa kuipinga serikali badala yake kuwa mshauri wa serikali katika shughuli za maendeleo.
“ Ni aibu kuona mtumishi wa umma anabadili uelekeo na kuwa mpinzani wa serikali kwa kuwapotosha wananchi na sitasita kumchulia hatua mtumishi huyo kwa mujibu wa sheria na taratibu za utumishi wa umma.” Mhe Chalamila
Chalamila amesema wataalamu wakiwa na agenda ya kuipinga serikali wanatakiwa kutoka katika sehemu ya serikali na kuwa wanasiasa ili kuendeleea kuipinga serikali katika majukwaa ya siasa.
Amewataka watumishi kusoma kanuni na taratibu za utumishi wa umma ili ziweze kuwaongoza katika utendaji kazi wao ili kuepuka mihemko ya kisiasa ambayo inaweza kusababisha migongano ya kimaslahi ya kiutendaji katika maeneo yao ya kazi,
Aidha, Mhe Chalamila amewataka watumishi wa taasisi za umma waliopewa mamlaka kutokuwa chanzo cha kuleta malalamiko au chombo cha kuwatisha wananchi kwa kuendelea kusimamia sheria na taratibu za serikali kwa kuwa waadilifu.
“Mnatakiwa kutoa huduma kwenye taasisi zenu kwa kuangalia sera na agenda ya nchi sasa ikiwa ni kuwahudumia wananchi kwa uadilifu ili kujenga uaminifu kwa wananchi mnao wahudumia” Mhe Chalamila.
Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bibi Mariam Mtunguja amewataka watumishi wa umma kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa kuwahudumia awananchi kwa taratibu, sheria na haki.
Bibi Mtunguja amesema kuwa wataalamu wa kiutendaji ndio wasaidizi wakuu wa Mkuu wa Mkoa katika kutekeleza majukumu ya maendeleo katika mkoa na hivyo ni muhimu kuwa na ushirikiano wa karibu katika utendaji kazi.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa