Jumla ya Wafungwa 259 Mkoani Mbeya wamekuwa miongoni mwa wafungwa Zaidi ya 5000 waliopatiwa msamaha wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kufuatia maadhimisho ya miaka 58 ya Uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika jana jijini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe Albert Chalamila amefika katika magereza ya Ruanda Na Songwe ambapo wafungwa 157 wamepatiwa msamaha WA Rais huku wafungwa wengine wakiwa katika Magereza ya Wilaya za Mbarali, Kyela na Rungwe na kuzungumza na wafungwa hao kabla ya kuondoka gerezani hapo.
“Msamaha huu uliopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haumaanishi umefuta makosa mliofanya hivyo vyombo vya dola vitaendelea kuwaangalia mtaani huko mnakokwenda, na tumejipanga zaidi kuangalia mienedo yenu hivyo mkapate shauku ya kuwa waadilifu huko mnakokwenda.” amesema Mhe Chalamila
Mhe Chalamila amewaagiza Wakuu wa Wilaya kuwapokea wafungwa hao wanaotoka Mkoa wa Mbeya na kuwakabidhi kwa Wakurugenzi wa Halmashauri ili wajiunge kwenye Vikundi na waweze kunufaika na mikopo inayotolewa na halmashauri kwa ajili ya kinamama, Vijana na watu wenye ulemavu.
Mhe Chalamila amewataka wafungwa waliobaki kuendelea kutafakari tabia iliyowapeleka gerezani na kuanza kubadilika ili msamaha mwingine utakapotokea wawepo miongoni ya watakaopata.
Mmoja wa wafungwa wa gereza la Ruanda Obed Mbuza amemshukuru Rais Magufuli kwa msamaha alio mpatia na kumuombea kwa Mungu aendelee kumlinda huku akieleza kuwa amejifunza mambo mengi alipokuwa gerezani na sasa anaenda kuwa raia mwema.
Bw. Ramadhan Shaban ambaye amepata msamaha wa Rais Magufuli amesema bahati aliyoipata ya Msamaha ataitumia vizuri kwa kufanya kazi halali kwakuwa Vijana wengi wamekuwa wakichagua kazi ambazo zinawaingiza katika matatizo
Ameongeza kuwa magereza ni sehemu ya urekebishaji na yeye amerekebika hivyo anawashauri vijana wote wafanye kazi halali ambazo hazitawaletea matataizo kwakuwa kazi halali zipo nyingi.
2 Barabara ya Kamishina, 53180 MBEYA
Anuani ya Posta: P. O.Box 754,Mbeya.
Simu: 025-2504045
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras@mbeya.go.tz
Haki Miliki©2023 Mkoa wa Mbeya. Haki zote Zimehifadhiwa